Home News Babutale asikilize maneno ya watu kuhusu Tip Top – Madee

Babutale asikilize maneno ya watu kuhusu Tip Top – Madee

Rapper Roma Mkatoliki aliiibua suala la meneja wa Tip Top Connection, BabUtale kutumia muda mwingi kwa kazi za Diamond na kusahau chimbo lake la zamani.
Madee ameibuka na kusema ‘lisemwalo lipo, kama halipo laja.’
“Tale anachotakiwa akifanye sasa hivi asikilize hayo maneno ya watu ayafanyie kazi sababu mwisho wa siku itakuja kuwa kweli, itakuja kutokea mtafaruku mwingine usiokuwa na mpango,” alisema Madee kwenye segment ya Mzee Kasema ya kipindi cha Funiko Base cha Radio 5.
Bado Tale hajawahi kujibu kwa uhakika kuhusu msimamo wake kuhusiana na kauli hiyo ya Roma iwapo ina ukweli.
Msikilize Madee hapo chini.