Home News Diamond ashirikishwa na staa wa Ivory Coast, Serge Beynaud

Diamond ashirikishwa na staa wa Ivory Coast, Serge Beynaud

Diamond Platnumz amegeuka kuwa msanii anayetafutwa zaidi na wasanii wa nchi mbalimbali Afrika kwaajili ya collabo.

Baada ya kushirikishwa na msanii wa Zimbabwe Jah Prayzah kwenye wimbo Watora Mari, mkali huyo ameshirikishwa kwenye wimbo mwingine na msanii wa Ivory Coast, Serge Beynaud.

Serge Beynaud
Kupitia Instagram, Serge ambaye pia ni producer mkubwa ameweka kipande kifupi cha wimbo huo.

            
Guy Serge Beynaud hufanya mtindo unaojulikana kama Coupé-décalé. Mtandao wa AllAfrica.com ulimwelezea Beynaud kama “Ivorian sensation” and a “heavyweight act”.