Home News Gabo Zigamba anusurika kifo katika ajali ya gari

Gabo Zigamba anusurika kifo katika ajali ya gari

Muigizaji wa filamu ya ‘Bado Natafuta’ Gabo Zigamba amenusurika kifo katika ajali ya gari wakati akielekea hifadhi ya Ruaha akiwa na wenzake wawili ambao wamejeruhiwa huku yeye akisalimika katika ajali hiyo.

Gabo amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki katika ajali hiyo.
“Uongo unaoishi ndiyo ukweli mpaka ukanushwe, nami naanzia hapa kwenye kukanusha, ni kweli nimepata ajali lakini sijafa na maumivu ni ya ndani sana,” aliandika Gabo katika istagram yake. “Na sijavunjika kama watu wanavyosema ila naumia na jinsi watu wanavyo waombea wenzio Mabaya,”
Aliongeza, “Nilikuwa na lengo zuri la kugawana umasikini na wanyonge wenzangu na hata Mungu akanisimamia. Eee Mollah wasamehe kwani na mimi nimewasamehe, naamini utaniongoza na kunisimamia leo, kesho na hata milele,”