Home News ​Mashabiki wa Wema Sepetu waushangilia uamuzi huu wa Diamond

​Mashabiki wa Wema Sepetu waushangilia uamuzi huu wa Diamond

Hakuna kitu ambacho mashabiki wa Wema Sepetu wanakipenda kama kuona kuwa kuna amani kati yake na Diamond.

Pamoja na kuwepo kwa tension kubwa kati ya wawili hao licha ya kila mmoja kuwa na hamsini zake sasa – yaani Diamond kuhamishia mabaha yake kwa Zari waliyejaaliwa mtoto wa kike, Tiffah na Wema kuwa mikononi mwa staa mwenzake, Idris Sultan, mambo yanaonekana kuanza kunyooka.
Jumanne hii Diamond aliwafurahisha sana mashabiki wa Wema pale alipoipromote show ya Black Tie iliyoandaliwa na Wema na Idris, July 9. 
Ikumbukwe kuwa wiki kama tatu zilizopita Wema alisikika kwenye mahojiano akimtupia lawama ex wake huyo kuwa alimfanyia fitina asiupate ukumbi kwa King Solomon kwaajili ya show yake hiyo ambapo Christian Bella atatumbuiza.
Kwa hatua hiyo huenda wawili hao wameamua kuyaacha yapite na wagange yajayo.

Post ya Diamond kuhusu show hiyo tayari imevunja rekodi kwa kuvutia comments nyingi zaidi. Hadi sasa zimefika takriban 5,000! Comments nyingi zinampongeza kwa uamuzi huo.
Naye Wema amepost picha mbili zilizokatwa na kuziacha kuanzia kidevuni kuja chini ambazo zinaonekana wazi kuwa ni picha za Diamond. Wakati wengi wakifurahia,upande mmoja lakini haujakipokea kikombe hicho cha chai – Team Zari!