Home News Jokate yuko busy na biashara, hatoonekana kwenye media na kuna hii ishu...

Jokate yuko busy na biashara, hatoonekana kwenye media na kuna hii ishu hata akiulizwa hatojibu

Pamoja na kuzungumzia ishu yake ya kupostiwa kwenye account ya Instagram ya mwigizaji na mwimbaji wa longtime wa Marekani Tyrese, Jokate amesema ‘hivi karibuni nimekua siongei sana na Media nimekua nafanya vitu vingi sana ambavyo havinipi nafasi, maswali ambayo sipendwi kuulizwa kuhusu maisha yangu binafsi
Hata ukiangalia page zangu za social media Instagram sipost Mchumba, sipost Wazazi na sipost ndugu kiviile kwa sababu najua ukiwapost unawaweka kwenye situation ya watu pia kuanza kuwaongelea na unajua watu wengi online wanaweza kuongea kitu chochote kile kwahiyo napenda kuwalinda watu ambao wako karibu yangu
Moja ya maswali ambayo ukimuuliza Jokate hatokujibu wala kuongelea chochote ni ishu ya uhusiano wake wa kimapenzi na mwimbaji Alikiba ambaye kipindi kilichopita tuliona wakipostiana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, kwa sasa Jojo anaonekana sana kupromote bidhaa zake za Kidoti, mtazame kwenye hii video hapa chini akiongea zaidi.