Home News Masanja asema Orijino Komedi imemalizana na polisi, ni issue ya kuvaa sare...

Masanja asema Orijino Komedi imemalizana na polisi, ni issue ya kuvaa sare za polisi

Baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuwakamata baadhi ya wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa kosa la kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Masanja Mkandamizaji amedai tayari wameshamalizana na jeshi hilo baada ya kuomba msamaha.

Mchekeshaji huyo ambaye kwa sasa yupo honey moon visiwani Zanzibar, amesema ameamua kutoa taarifa hiyo ili kuwaondoa hofu baadhi ya mashabiki pamoja na ndugu.
“Jamani asanteni kwa maombi na meseji zenu kuulizia juu ya inshu ya polisi, tunamshukuru mungu tumewaomba msamaha na wametusamehe hivyo imekwisha,” aliandika Masanja facebook.
Aliongeza, “Tumesema tulinogewa na harusi tukasahau kwenda kuomba kibali. Lakini akina Joti, Seki, Maclegan,na Wakuvanga wamepata kautamu kidogo kamahojiano. Na mimi ningekuwa kwenye jiji la Makonda ingenihusu,”
Wasanii hao walikamatwa na jeshi la polisi na kuhojiwa baada ya kuvaa sare zinazofanana ya za jeshi la polisi katika harusi ya msanii mwenzao Masanja Mkanadamizaji.