Home News ‘Mashabiki ndiyo watakaonipa tuzo’ Bright

‘Mashabiki ndiyo watakaonipa tuzo’ Bright

Msanii Bright ambaye anawania tuzo ya msanii bora chipukizi kwenye #EATVAwards, amesema ana imani mashabiki wake ndiyo watakaompa ushindi, kutokana na suport kubwa anayoipata kutoka kwao.

Akizungumza kwenye kipindi cha 5SELEKT cha EATV, Bright amesema anaamini mashabiki wake watambeba kwenye kupiga kura na hatimaye kuweza kuwabwaga wasanii wenzake kwenye kipengele hicho, kwani wao ndiyo watu wa mwisho wenye maamuzi juu yeye kushinda au la.
“Nina fanbase kubwa sana, mashabiki wangu wanaona kazi yangu wananikubali, na nina imani wao ndiyo watanifanya nishinde kwa kunipigia kura, kwani siku zote wananiunga mkono kwenye kazi zangu”, alisema Bright.
Bright ambaye mpaka sasa ana kazi moja tu ambayo ndiyo imemfanikisha kupenya kwenye #EATVAwards, amesema anajiamini kuwa atashinda tuzo hizo, ingawa kwake ni changamoto kubwa.
“Najiamini kwanza nafanya kitu kikubwa, watu wanajua, watanzania wanajua kuwa nafanya kitu kikubwa, kwa hiyo ni uaminifu tu kwa sababu biashara yangu ina uzika, lazima niipeleke sokoni.
Pia Bright amewataka wasanii wengine chipukizi kuwa na uthubitu na kuishi katika ndoto zao kwa vitendo.