Home News Nay wa Mitego azungumza baada ya BASATA kumfungia

Nay wa Mitego azungumza baada ya BASATA kumfungia

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amewaambia mashabiki wake kuwa atawakumbuka sana baada ya hapo jana Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA kutangaza kumfungia msanii huyo kwa muda usiojulikana.

Rapper huyo amekutana na rungu hilo la kufungiwa baada ya kuachia wimbo ‘Pale Kati’ ambao mashairi yake yameonekana kukosa maadili na pia msanii huyo hajasajiliwa na baraza hilo la sanaa.
Kupitia akaunti yake ya instagram, Nay ameandika, “Daaaaah..!! Nitazimiss sana hizi Show..!!😂😂😂😂😂🏃🏿🏃🏿🏃🏿
#PaleKati 🏃🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿.”
“Paka akitoka, Panya hutawala..!! Sasa akirudi watatafuta pakujificha ni kuwatafuna tu!! 🏃🏿🏃🏿
#PaleKati,” 
ameandika kwenye picha nyingine aliyoiweka kwenye mtandao huo.