Home News Oscar Pistorius atwangwa miaka sita jela

Oscar Pistorius atwangwa miaka sita jela

Mwanariadha mlemavu wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa hatia ya kumuua mpenzi wake.

Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake huko Pretoria kwenye Valentine’s Day, miaka mitatu iliyopita – tukio ambalo amekuwa akisisitiza kuwa ni bahati mbaya kwakuwa alihisi ni jambazi.
Upande wa mashtaka ulisisitiza kuwa mwanariadha huyo na mpenzi wake walijibizana kabla ya tukio hilo.
Mwaka 2014 jaji huyo huyo alimhukumu Pistorious kwa kosa la kuua bila kukusudia lakini mahakama kuu iliibadilisha kesi yake kuwa ya kuua kwa kukusudia na hatimaye hukumu mpya kutolewa Jumatano hii.
Hiyo itakuwa ni hukumu ya mwisho ya kesi hiyo ya miaka kadhaa sasa.