Home News ​Polisi wanne wauawa Marekani, ni kufuatia mauaji ya watu wawili weusi

​Polisi wanne wauawa Marekani, ni kufuatia mauaji ya watu wawili weusi

Polisi wanne wameuawa mjini Dallas wakati makundi ya watu yakiandamana kupinga kuuawa kwa wamarekani weusi wawili huko Louisiana na Minnesota.

Polisi wa Dallas wamesema maofisa 11 walipigwa risasi.
Washukiwa wa mauaji hayo walitishia kutega bomu mtaani.

Tukio hilo limekuja baada ya polisi kuwaua watu weusi wawili katika matukio tofauti. Philando Castile aliuwa akiwa kwenye gari huko Minnesota na Alton Sterling Louisiana aliyeuwa wakati akiuza CD kwenye eneo la kuegesha magari.
Watu maarufu akiwemo Beyonce wameendelea kupaza sauti zao kulaani mauaji hayo.