Home News Rockstar4000 waeleza kwanini Alikiba ameamua kufanya birthday party kubwa mwaka huu

Rockstar4000 waeleza kwanini Alikiba ameamua kufanya birthday party kubwa mwaka huu

Ni nadra kuona Alikiba akifanya sherehe kubwa kwaajili ya birthday yake.
Lakini mwaka huu muimbaji huyo wa Aje aliamua kufanya kitu tofauti.
Nimeuuliza uongozi wake sababu ya mwaka huu kufanya sherehe kubwa na tena mbugani. “Yes ni mara chache hufanya party on his birthday,” amesema mmoja wa mameneja wake.
“Aliamua kuja mbugani kwa sababu kuu ni kwa sababu anapenda wanyama pili ni kutumia jina lake kutangaza utalii wa ndani,” aliongeza.
Wafanyakazi wa makampuni mbalimbali ya mbugani yaliungana na uongozi wake kusherehekea siku yake hiyo muhimu ambayo ametimiza umri wa miaka 30.
Chini ni picha zaidi za party hiyo.