Home News Utani wa Idris Sultan kwa Diamond na Zari

Utani wa Idris Sultan kwa Diamond na Zari

Kama huwezi utani basi jiweke mbali na Idris Sultan kwa kuwa ipo siku unaweza kujikuta ukifanya kitu usichokitarajia.
Mchekeshaji huyo ameandika ujumbe wa utani kwa Diamond na Zari kwenye mtandao wake wa Instagram baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa kuwa First Lady huyo wa WCB alikuta hereni kwenye chumba cha Diamond ikionekana kuwa alimsaliti na mwanamke mwingine.
β€œNdio imeingia na DHL @diamondplatnumz nakupitishia hapo maana umepoteza control mambo yanamwagika hovyo mara hereni ulizisimamia kama kangaroo,” ameandika Idris kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.
Hakuishia hapo Idris amempongeza Zari The Bosslady kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuweka picha ya hereni kwenye mtandao huo na kuandika ujumbe unaosomeka, β€œHappy birthday @zarithebosslady πŸ˜….”