Home News Video: Diary ya Alikiba yaanza kuonekana Rockstar TV

Video: Diary ya Alikiba yaanza kuonekana Rockstar TV

Alikiba amezidi kuwafurahisha mashabiki wake – ameanza kutekeleza kati ya ahadi tano alizoahidi.alikiba

Ni muda mrefu mashabiki wamekuwa na kiu ya kuona vitu vya Alikiba anavyoahidi kuchelewa utekelezaji wake, sasa ameanza kutekeleza moja ya ahadi zake ikiwa ni kuanza kuonesha baadhi ya sehemu ya maisha yake aliyowahi kupitia kwenye muziki kupitia Rockstar Television.
Kwa kuanza kuonyesha maisha aliyowahi kupitia hitmaker huyo wa ‘Aje’ ameanza kuonyesha maisha ya muziki aliyowahi kupitia kwa kuonyesha alivyokuwa studio na wasanii wengine wa Afrika pamoja na R Kelly wakati wanarekodi wimbo wa ‘Hands Across The World’ mwaka 2010.