Home News Wewe ni underground? Ujumbe huu wa Rich Mavoko utakupa moyo

Wewe ni underground? Ujumbe huu wa Rich Mavoko utakupa moyo

Historia za wasanii wengi waliofanikiwa zina mambo mengi ya kusisimua.
Wengi wamepitia vikwazo vingi lakini ni wale waliovumilia tu ndio ambao hadi leo wapo na wamefanikiwa sana. Rich Mavoko ameshare kwa ufupi yale aliyopita kwenye safari yake ya muziki na kutoa ushauri muhimu kwa wasanii wachanga wanaohangaika sasa.
Akiweka wimbo wake wa kwanza kwa kuufanyia video, Mavoko aliandika:
Huu ndo ulikuwa mwanzo wangu mwaka 2010 nilitoa hii kazi ilikuwa ina vikwazo vingi sana ila tukafanikisha locaction kuzingua kwa msanii uliyefanya nae kazi kutompata kwa muda unaotakiwa ila tulimaliza Mtu ambaye alifanyikisha hii kazi ni rafiki yangu Rama na Mwenzake Hk haikuwa rahisi kabisa kama tunavyoiona na mpaka kumpata model pia ilikuwa swala jingine sababu nilikuwa natamani kufanya nae kazi kwa wakati huo nae alikuwa wa moto sana lulu ila tukafanikisha ila usichokijua kwenye hii video ndoto yangu kubwa nilitaka kufanya na Adam juma swala lilikuwa gumu kwa kipindi icho kipato kilikuwa kidogo ikabidi adam atupe mejja ambae alikuwa visual lab hapo hapo tukashukuru ila mimi moyo wangu nilitamani sana Adamu juma ndo ilikuwa ndoto yangu kubwa kufanya nae kazi..
Sikuchoka kujitaidi hatimae video yangu ya silali nikafanya na alAdam juma pia ni kazi ilikuwa ina matatizo mengi ambayo kiubinadam sipaswi ya sema namshukuru sana Adam alilimaliza swala ili likiwa limekaa sawa… rehemvisulab pia siwez msahau alichangia mengi kwenye safari yangu ya kufanya harakati za kushoot ili nifunzo kwa vijana ambao wanatamani kuwa wasanii wa mziki huu una vikwazo usije ukawa mtu wa kulalamika mana kumbuka ivi vitu aviji kirahisi kudharaulika ni kawaida sana tena usije ukasusa mana haitokusaidia kaza mana safari yake kuna mawili kupata au kukosa ila moyoni mwako jiekee kupata ili uwe na moyo ata pale unapokesea kwamba ufanye kwa bidii ipo siku kuchoka kwenye kazii hii ni mwiko pia ni kazi ambayo inahitaji uwe mpole sana mana kila mtu atatamani kukuelezea tofauti mara unaringa pale unapo onekana unapata so ishi nao vizuri jaribu ata kujishusha ishi kama bwege na kuheshim ata kitu kidogo ambacho unaambiwa ingawa mda mwingine unaona kabisa ichi sio ila sikiliza mana kwenye maneno kumi utakayoambiwa uwenda kuna ukweli ata robo au nusu.
Hivi karibuni Mavoko alisainishwa na label ya WCB na kuachia wimbo wake, Ibaki Story.